Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Jawadi Amuli amefafanua sehemu mbalimbali za Swala ya maiti iliyoswaliwa juu ya Kiongozi Shahidi.
Amesema: "Ikiwa mmetilia maanani, sisi (katika Swala ya maiti ya Kiongozi Shahidi) tulitenganisha mpaka wa ushahidi na mpaka wa kuuawa kwa kawaida. Shahidi kwa maana ya jumla ni kama ilivyo katika Hadithi:
«مَن قُتِلَ دُونَ مَظْلِمَتِهِ فَهُوَ شَهِیدٌ».
Riwaya hizi ni za jumla. Ikiwa mtu atauawa akiwa katika njia ya haki, au atauawa kwa ajili ya kulinda mali yake, au atauawa kwa ajili ya kulinda heshima na mipaka yake; kama ilivyo katika Hadithi:
«مَن قُتِلَ دُونَ مالِهِ ظُلماً فَهُوَ شَهِیدٌ».
basi huyo ni shahidi kwa maana pana.
Lakini shahidi kwa maana maalumu, ambapo tunasema mtu huyu ni shahidi, anatofautiana na maiti wa kawaida.
Kwa hiyo, katika Swala (Swala ya maiti ya Kiongozi Shahidi), pale ambapo kulikuwa na bahathi kuhusu kuulinda Uislamu, Qur'ani na Ahlul-Bayt (as), na juhudi kubwa za shahidi huyu mtukufu (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) pamoja na wenzake, alitajwa kwa sifa ya 'Shahidi'.
«اللهم، اللهم، اللهم إنه نزل عندک شهيداً للإسلام والقرآن والعترة»
Ama pale ambapo mazungumzo yalihusu kulinda uhuru wa Iran, taifa la Iran, uchumi wa Iran, mipaka ya Iran na mambo kama hayo, alitajwa kwa neno 'Qatīl (Mwenye kuuwawa)'.
«اللهم، اللهم، اللهم إنه نزل عندک قتيلاً للإسلام، قتيلاً للأمة المسلمة، قتيلاً لسياستها، قتيلاً لصيانتها، قتيلاً لكيانها، قتيلاً لعظمتها وسيادتها ومولويتها ووحدتها»
Shahida kwa maana ya jumla inajumuisha mambo yote haya, kwa sababu kanuni ya msingi ni hii:
«مَن قُتِلَ دُونَ حَقِّهِ فَهُوَ شَهِيدٌ»
Lakini sasa wajibu wetu ni upi mbele ya Walii al-Faqih?
Yule mtukufu ambaye sasa ameketi mahali pake, (Mwenyezi Mungu amlinde), ni mtu mwema aliyerithi nafasi ya mwema. Kwetu sisi, anakubalika kikamilifu kuwa amekaa mahali pake, anaendeleza fikra zake na anatekeleza kazi zake.
Wajibu wetu ni kumuunga mkono; kama tulivyokuwa tukimuunga mkono yule mtukufu. Vilevile, wajibu wetu ni kumlinda; kama tulivyokuwa tukimlinda yule mtukufu, huo ndio wajibu wetu."
Maoni yako